Abakwa na midume kumi

Ukimuona tu utagundua kuwa mama huyu wa haja aliyejitambulisha kwa jina la Winfrida Juma ana madhila mazito yanayomkabili maishani. Sura isiyo na chembe ya furaha, machozi yenye kutiririka kila wakati na cha kusikitisha zaidi ni mwendo wake wa kuchechemea unaoashiria maumivu makali.
’’Nimekuja mniandike ili walau niweze kupata msaada kwa wasamaria ama ndugu na jamaa wasiofahamu balaa lililonikuta,’’ ndivyo anavyoanza kuzungumza mama huyu anayedai kuwa na watoto watatu, mkazi wa Kitunda kule kwenye maeneo ya Ukonga jijini Dar es Salaam. Ni yepi hayo yaliyomsibu? ’’Nimebakwa na wanaume kadhaa hadi ni kazimia...nilipoamka masaa mengi baadaye nikajikuta nikiwa hoi katika kituo cha Polisi Mabatini.
’’Baadaye mume wangu naye akanitimua na kusema kuwa hanitaki tena kwa sababu nimeharibiwa vibaya baada ya kubakwa,’’ ndivyo anavyoendelea kusimulia mama huyu huku akibubujikwa na machozi. ’’Hivi sasa nimehifadhiwa tu na msamaria mwema mmoja ambako najiuguza kwa majimoto na dawa nyingine za kienyeji ili kupunguza majeraha. Nashindwa kwenda hospitali ama popote pale kwa sababu fedha sina.
Hicho nd’o kilichonileta kwenye gazeti lenu,’’ anasimulia zaidi mama huyo. Ilikuwaje mpaka akakumbwa na balaa hilo la kusikitisha lililotokea hivi karibuni? ’’Siku ya tukio nilitoka nyumbani kwangu mida ya jioni na rafiki yangu mmoja ili kwenda kumtazama mgonjwa ambaye ni mjomba wa rafiki yangu huyo.
Tulipotembea kwa muda mfupi tu, tukawakuta majirani zangu katika nyumba moja wakinywa pombe, wakatukaribisha na siye tupate kidogo kabla ya kuendelea na safari. Mie na mwenzangu tukakubali na kujiunga nao katika kinywaji,’’anasimulia Winfrida.
Akiendelea kusimulia zaidi, mama huyo ambaye anadai watoto wake watatu wana umri wa miaka 9, 7 na mitatu anasema:
”Wakati tukiendelea kuburudika, mara kukatokea mtafaruku kati ya yule rafiki yangu niliyekuwa nikiongozana naye na mmoja kati ya majirani waliotukirimu pombe. ’’Kwa sababu hiyo, yule rafiki yangu akaondoka mahala hapo ghafla na kuniacha mie nikiendelea kupata kinywaji na wale waliotukaribisha.’
’ Halafu ikawaje?
’’Mara nikashikwa na haja ndogo na kulazimika kuacha bia yangu kwa muda na kwenda msalani. Niliporejea, hakuna nilichofanya zaidi ya kuimalizia ile bia niliyoacha. Mara, nikahisi kichwa kinakuwa kizito, kizunguzungu na mwishowe nikapotewa na fahamu.
Sikujua tena ni kitu gani kinaendelea. Hiyo ilikuwa ni kenye mishale ya saa 10:00 hivi. ’’Nilipokuja kustuka mishale ya saa 10:00 alfajiri, ndipo nikashangaa kwa kujikuta nikiwa kwenye kituo cha polisi. Nilipojaribu kujigeuza, nikahisi maumivu makali sana sehemu za siri na nilipojiangalia, nikajikuta nikilia kwa uchungu na hofu.
Tayari nilikuwa nimeharibiwa vibaya baada ya kubakwa na wanaume ambao kwa vyovyote vile walikuwa wengi na tena walipania hasa kuniangamiza kwa njia hii...inaniuma sana kwakweli,’’ akasema Winfrida. ”Baada ya hapo nikalia sana kwa maumivu...askari mmoja akanichukua na kwenda kuniangalia vizuri. Ndipo hapo akaona ni namna gani nimeharibiwa vibaya na wabakaji.
Nikapewa PF3 na RB ya kuwakamata watuhumiwa ambao kwa bahati, walipatikana na kushikiliwa polisi Mabatini. ’’Mimi nikalazimika kujingoja hadi nyumbani ili nionane na mume wangu, kisha kwa msaada wake niende hospitalini kutibiwa wakati suala la walionifanyia unyama huo likiendelea kushughulikiwa kisheria.’’ Kufika kwa mumewe ikawaje? ’’Sikuamini. Licha ya kumueleza kwa undani juu ya mkasa ulionipata, mwenzangu hakutaka kunielewa na alichokifanya ni kukataa kunipokea na kunitimua.
Kwakuwa hali yangu sio nzuri, nikalazimika kujikongoja hadi kwa jirani yetu mmoja na kujihifadhi hapo wakati nikijaribu kusaka uzima kwa njia ya dawa asilia...sina senti za kuniwezesha kwenda hospitalini. Nikimpata wa kunisaidia kwa jambo hilo nitashukuru sana,’’ akasema mama huyo.
Wakati mwandishi wa habari hii hakuweza kupata maelezo mengineyo kwa mama huyo kutokana na hali aliyo nayo kumfanya asiwe katika hali nzuri ya kuzungumza sana, Komesha litaendelea kuripoti kwa undani endapo kutakuwa na jipya katika tukio la mama huyu, hasa kutokana na ukweli kuwa si mume wala majirani waliozungumzia sakata hil

0 Comments:
Post a Comment
<< Home