Mchungaji asomea waumini misa ya wafu
Mchungaji Mosha wa kanisa la Ark Fondation lililoko Kimara Baruti, anadaiwa kuwasomea misa ya kifo waumini wake zaidi ya 15 hivi ambao wako hai kwa madai ya kuhudhuria harusi ya watu ambao si wa dhehebu hilo, yaani hawajaokoka.
Pia Mchungaji huyo anadaiwa kuwaambia kuwa waumini hao kuwa wamekufa kimwili na kiroho na ndiyo maana ameamua kuwasomea misa hiyo ambayo ni maalum kwa kuwasomea watu waliokufa tu. Sambamba na tukio hilo, hivi sasa waumini hao wametengwa na kanisa hilo kwa kitendo chao hicho na kuambiwa na mchungaji huyo kuwa hata kama watakwenda kwenye dhehebu lingine, lakini dhehebu hilo litakuwa linapokea watu waliokufa na si hai.
Waumini hao ambao majina yao tunayo, wameeleza kusikitishwa kwa kusomewa misa wanayosomewa marehemu, pamoja na mchungaji huyo kuwasalia sala ya kifo ambayo ni maalum kwa watu waliokufa tu na wakati wao wako hai. ’Sisi tuko hai, lakini tumesaliwa misa ya wafu na sala ya marehemu na tunaambiwa kuwa tumekufa, hii sisi inatutia wasiwasi sana wa maisha yetu, hatumuelewi huyu mchungaji ana maana gani au nia gani,’ alisema mmoja wa waumini hao.
Wakisimulia mkasa mzima ulipoanzia hadi wao kuambiwa kuwa ’wamekufa’, wamesema kuwa kuna binti mmoja ambaye ni mmoja waumini wa kanisa hilo anaitwa Agahta Mlay alipata chumba ambaye si wa dhehebu hilo yaani si mlokole, lakini alipomwambia mchungaji huyo kuwa anataka kuolewa na mwanaume huyo, mchungaji Mosha alikataa katakata ndoa hiyo na kudai kuwa itakuwa ni batili kwa kuwa mwanaume huyo bado hajaokoka.
Hata hivyo, wakadai kuwa wao kama waumini akashangaa kwani si siku nyingi zilizopita, mchungaji huyohuyo alimuozesha binti yake aitwaye Oliver kwa kijana ambaye si mlokole. ’Mchungaji alihudhuria harusi hiyo ambayo pia ilikuwa na vinywaji kama vile pombe, lakini hakukataza wala kusema ni batili, tukashangaa kwa nini alimkatalia binti huyo,’ alisema mmoja wa waumini hao.
Waumini hao wakasema kuwa, binti huyo kuona hivyo hakusikiliza tena ya mchungaji ang’ang’ania kuolewa, kiasi cha mchungaji kuamua kumfukuza na kumtenga, pia akaamuru waumini wote wa kanisa lile kutoshirikiana naye kwa kuwa amekiuka maagizo ya Mungu ya kuolewa na mtu wa ’mataifa’ ambaye hajaokoka na kumrudia Bwana.
Hata hivyo, wakasema kutokana na kuonekana kama kuna kaubaguzi, yaani Agatha akataliwe kuolewa na mtu ambaye ni mlokole na Oliver akubaliwe kukaleta mgawanyiko kwenye kanisa hilo, ambapo wao waliamua kumuunga mkono Agatha kwani akinamama alikwenda kwenye ’kicheni pati’ yake na baadaye wake kwa waume walihudhuria harusi hiyo yake. Waumini hao wakasema kuwa kasheshe lilianza pale mchungaji alipopata habari kuwa kuna baadhi ya waumini wake walihudhuria harusi ya binti aliyemtimua kwenye kanisa lake.
’Waumini walipokusanyika kanisani siku hiyo ndipo alipowatangazia kuwa kuna watu walihudhuria harusi ya Agatha ambaye alitengwa na kanisa, hivyo na wao hawafai kuwemo katika Kanisa na pia na wao wamekufa kimwili na kiroho kwa hiyo na lazima tuwasalie misa maalum ya wafu ikiendana na sala ya marehemu na hata wakipokelewa na madhehebu mengine basi wajue wanapokea watu waliokufa,’ alisema muumini mwingine.
Akijibu tuhuma hizo, Mchungaji Mosha amesema kuwa ni kweli waumini hao wamekufa kiroho kwa mujibu wa maandiko matakatifu na si kwa mujibu wake yeye kama mchungaji Mosha. Akasema kuwa watu ambao wamekiuka maagizo ya mwenyezi Mungu kwenda kwenye harusi batili ya mtu anayezini kwa makusudi wakati tuliwatangazia, ni sawa na mtu aliyekufa kiroho. ’Ni kweli tulitaka kuwasomea misa ya wafu, yaani watu waliokufa kiroho, lakini kabla hatujafanya hivyo baadhi yao wakaja kutubu kwa hiyo tukasimamisha na mpaka sasa bado hatujasoma misa hiyo,’ alisema mchungaji huyo.
Akatetea hoja hiyo kwa kusema kuwa katika maandiko matakatifu kuna ibada ya mazishi ya watu waliokufa kiroho na ibada ya ufufuo wa watu waliofufuka kiroho, kwa hiyo waliokufa kiroho watasomewa na waliofufuka kiroho watasomewa tu na kuongeza kuwa watu waliokuja kutubu anatarajia kuwasomea ibada ya ufufuo wa kiroho kwa sababu wamekuja kutubu na kuona walilofanya ni kosa kwa Mungu.
Akasema Agatha alipata mchumba ambaye hajaokoka na kutaka kufunga naye ndoa na katika kumbana alikiri kuwa mchumba huyo anaye kwa muda wa miaka mitatu sasa. ’Mlokole ana mchumba kwa miaka mitatu huko nje, anakuja kusali anajifanya mlokole, kumbe akitoka anakwenda kuzini nje, huyo mtu kweli tukimtenga kweli kuna kosa?,’ akahoji mchungaji. Akasema hata wa wazazi wa binti huyo walimtaka kwanza kijana huyo aokoke ndipo amuoe binti yao, lakini ikashindikana.
’Wakaja kwangu mimi nikawaambia msimamo wa kidini ni kuwa kama kijana hajaokoka hakuna ndoa, lakini nashangaa baada ya siku kadhaa wazazi wenyewe wakaelewana, wakaja kunidanganya kuwa kijana huyo eti ameokoka, sijui wapi, nikawaambia kwa nini hakuja kuokokea hapa ili niwape kibali cha kuoana, hawakujibu kitu.
Nikarudia msimamo wangu kuwa ndoa hiyo ni batili, na kuanzia wakati huo nikawaambia kama watafunga ndoa basi kanisa litakuwa limemtenga na nikawaarifu waumini wote wa Kanisa langu wasishiriki kwa njia yoyote ile kwenye maandalizi au sherehe la sivyo naye atatengwa na watakufa kiroho, lakini baadhi yao ndio hao waliokwenda,’ alizidi kudai mchungaji huyo.
Hata hivyo alikanusha kuwa binti yake ameolewa na mtu ambaye hajaokoka na kusema hiyo siyo kweli na hizo ni njia zao za kujitetea tu na kumalizia kuwa neno la Mungu na maagizo yake yatabaki pale pale na hakuna wa kupindisha kwa sababu ya kumpendezesha mtu.

2 Comments:
Habari kubwa hii.Hivi hawa wachungaji hewa wanatokea wapi?Nani kasema kuna mtu ana haki zaidi ya mwenzake mbele za mungu?
[color=#475]
Как дела? Может-быть... есть cупер предложение по[url=http://www.pi7.ru] видео[/url] порталу Думаю вам понравится
[url=http://www.pi7.ru]гланды кончаешь в горло [/url]
aнекдот для разнообразия :)
Онеа и он. Она:
- Хочусекса... Ну очень хочу! На 2 часа не меньше! Вот ты можешь два часа?
- Нв коенчно могу!
- А можно нескромный опрос... ыТ букдешь во время секса кричать?
- Да, от уужааса...
- Почему
- Потому, что я жуе всё, а до кгнца секса ещё 1 час 50 минуу!т
Я 5 часмов блуждала по сети, пока не вышкла на ваш форуп! Думаю, я здесь останусь надолго!
прошу прощения за опеатик.... чоень маленькая клавиатуа у PDA!
[/color]
Post a Comment
<< Home