Thursday, August 18, 2005


Jana baada ya kutoka kazini nilienda Muhimbili kumcheck my sister she was admitted there alijifungua kwa operation mtoto akawa bahati mbaya.Akaruhusiwa kurudi home but after three days hali yake ikaanza tena kuwa mbaya ikabidi wamrudishe tena hospitali Muhimbili kwa ajili further checkup.

Madaktari wa muhimbili ni wazembe sana na kimsingi hawana utu kabisa kumbe wakati walipomfanyia operation walitoboa mfuko wa uzazi sasa ile damu ambayo iko supposed kutoka kwenye uterus to go out ikawa inaingia tumboni na kuweka kibwawa hapo.I thanks God kwamba walimfanyia tena operation nyingine wakanyonya ile damu chafu na mpaka jana naondoka alikuwa bado hajitambui lakini na imani atapona.

Sasa basi niwaeleze mkasa niliyo uona huko hiyo jana yaani ni mambo ya kutia simanzi na kukatisha tamaa.Baada tu ya kutoka nje tukijiandaa kuondoka mara ikaja pajero moja ambayo ina mtazamo wa ambulance ilitolewa msaada kwa ushirikiano na watu wajapan.Ndani ilikuwa imembeba dada mmoja kalazwa kwa nyuma sio kwenye seat ni sehemu ya wazi.

Mbele alikuwa amekaa nesi mmoja mwenye sare nyeupe amebeba kitoto kichanga nadhani ni cha huyo dada.Huyo nesi akashuka akikiwaisha kichanga ndani.Mara akaja nesi mwingine amevaa sare ya Orange hivi akamchungulia yule dada kwenye gari akasema ‘mimi siwezi kumhudumia huyu si kaja na nesi wake kwani yeye akujua siku zake zimefika’huyoo akarudi ndani.

Zikapita kama dakika kumi hivi akarudi tena akamuliza yule dada aliyelazwa kwenye gari ‘Nguo zako za kujifungulia ziko wapi? Yule dada akajibu kishida shida ‘sina’...sasa wewe unakuja hapa nguo huna unategemea nini nyanyuka hivyo hivyo na midamu yako tukupeleke wodini’ akawa anamfokea.

Ikabidi yule dereva wa lile gari amsihi akamchukulie hata shuka ndani yule nesi akarudi ndani kuchukua shuka.Akaja na kiti cha kusukuma akafungua mlango wa nyuma akamtupia shuka akamwamuru ashuke mwenyewe akae kwenye kile kiti...imagine yule dada katoka kujifungua hata nguvu hana ashuke kwenye gari na akae kwenye kile kiti peke yake jamani...!!

Ok yule dada akajitahidi kushuka huku akiwa uchi kabisa anavuja madamu (samahani) huko chini kuna linyama linaninginia hata nguvu hana akajiachia hata kwenye kiti akuweza kukaa akadondoka ikabidi waje manesi wengine wenye sare za orange kusaidiana kumbeba wakampakia kwenye kitanda cha wagonja na sio kiti tena.


Wakamuingiza ndani huku wanamshushia matusi ‘ulivyokuwa unatoa uliona raha eeh..ooh mwanamke unakuwa lazy lazy namna hii sijui nini maneno kibao mpaka wanaingia naye ndani sijui sasa nini kiliendelea.Ndio ikabidi nimfuate yule dereva na kuliza kwani mmemtoa wapi huyu dada.Akasema yule dada alikuwa reception muda mwingi sana anasubiria kuhudumiwa akajisikia kubanwa na mkojo wakati anaenda kukojoa mara akamsukuma mtoto badala ya mkojo kitoto kikadondoka hapo barabarani ndio ikabidi wamchukue na kumleta pale wodini’..akamaliza kutuelezea.

Ndugu zangu nataka tu niwambie kitu kimoja kuwa Pale muhimbili kama huna mtu wa karibu unayemfahamu au huna pesa usiende otherwise unless utakufa.

Nimemaliza.

2 Comments:

At 4:40 AM, Anonymous Anonymous said...

Waswahili nyie ni watu wa ajabu sana. Mnazungumza hata vitu msivyovijua. Unasema madaktari wa Muhimbili ni wazembe halafu wewe mwenyewe unasema wakamu-operate tena mgonjwa wako halafu akapona.

Kwanza kufanya makosa wakati wa kufanya operation sio kitu cha ajabu. Madaktari sio miungu. Si ulisikia wale akina dada wa Iran!

Ndugu yangu udaktari hasa Tanzania ni kazi. Mbona hukuwatetea madaktari wakati wanatetea madai yao. Je, hujui kwamba wengine hufanya kazi wakiwa na matatizo ya kimaisha lukuki ambayo aghalabu yamesababishwa kwa mishahara midogo waipatayo?

Unalaumu tu, wakati wewe mwenyewe umesema umeona ambulance ambayo ni msaada toka Japan. Je, hao wadaktari wanavyo vifaa? Unajuaje kwamba huko kuvuja kwa damu kulisababishwa na ukosefu wa vifaa?

Ndugu udaktari sio kujua kuchora uterus tu! Hilo ni kama tone moja la maji ndani ya bahari. Umeandika mambo mengi kwenye habari yako lakini ni non-medical.

Waangalieni jinsi madaktari wanavyohudumiwa kabla hamjawalaumu. Laiti ungejua yapasayo.....

 
At 10:13 AM, Anonymous Anonymous said...

nakuunga mkono,manesi na wahudumu wa muhimbili wanakahuri chafu sana, kwny vinywa vyao cha kushangaza,pia ni wazazi, ni wanawake wenzetu, hawana huruma,na wanawake wenzeo, chakushangaza mbona wao walizaliwa kwa njia hiyo,
kama unavyosema, huyo dada hakuwa na nguvu,baada ya kumpa huduma haraka, jamani nyinyi manesi wenye kauli chafu, kafanyani kazi,machinjioni tujuwe moja,mumakera muna, kumbka dawa yenu iko jikoni,na tunawajuwa kwa majina. kumbukeni mlipo kula kiapo, cha ukarimu, na upendo, manesi wa wamuhimbili,jirekebisheni, ni wazazi wa ngapi wanapoteza maisha kwa uzembe wenu,fanyeni kazi kama mlivyoisomea taaluma yenu, asante sana uliyeandika kisa hicho,hiheshimuni kazi yenu na kuipenda manesi kitengo cha wazazimuhimbili

 

Post a Comment

<< Home

WAGONJWA WA KANSA
WAGONJWA WA KANSA
Niandikie